KANUNI YA IMANI



Nasadiki kwa Mungu Mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia, na Yesu Kristu, Mwanae wa pekee, Bwana wetu, aliyetungwa na Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasulibiwa, akafa na akazikwa; akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele.

Amina.