Sala ya Nasadiki



Nasadiki kwa Mungu mmoja,
Baba mwenyezi,
muumba wa mbingu na dunia,
na vitu vyote vinavyoonekana, na visivyoonekana.

Nasadiki kwa Bwana mmoja, Yesu Kristu,
Mwana wa pekee wa Mungu,
aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote,
Mungu aliyetoka kwa Mungu, Mwanga kwa Mwanga,
Mungu kweli kwa Mungu kweli,
aliyezaliwa bila kuumbwa,
mwenye Umungu mmoja na Baba.

Ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.

Alishuka kutoka mbinguni,
kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu:
Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu
kwake yeye Bikira Maria,
akawa mwanadamu.

Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi
akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato;
akafa na akazikwa.

Akafufuka Siku ya tatu
kadiri ya maandiko;
akapaa mbinguni
ameketi kuume kwa Baba.

Atakuja tena kwa utukufu
kuwahukumu wazima na wafu,
na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,
Bwana mleta uzima,
atokaye kwa Baba na Mwana.

Anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana.

Aliyenenwa kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa kanisa moja,
takatifu, katoliki, la mitume.

Naungama ubatizo mmoja
kwa maendeleo ya dhambi.

Nangojea na ufufuko wa wafu,
na uzima wa milele ijayo.

Amina.