Litania ya Loreto

Bwana utuhurumie.
Kristu utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Kristu utusikie.
Kristu utusikilize.
Baba wa mbinguni, Mungu,
utuhurumie.
Mwana, mkombozi wa dunia, Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja,
Maria Mtakatifu, utuombee.
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Bikira Mtakatifu Mkuu wa mabikira,
Mama wa Kristu,
Mama wa kanisa,
Mama wa neema ya Mungu,
Mama mtakatifu sana,
Mama mwenye usafi wa moyo,
Mama usiye na doa,
Mama usiye na dhambi,
Mama mpendelevu,
Mama mstaajabivu,
Mama wa shauri jema,
Mama wa Muumba,
Mama wa Mkombozi,
Mama wa huruma,
Bikira mtaratibu,
Bikira mwenye heshima,
Bikira mwenye sifa,
Bikira mwenye enzi,
Bikira mwenye huruma,
Bikira amini,
Kioo cha haki,
Kikao cha hekima,
Sababu ya furaha yetu,
Chombo cha neema,
Chombo cha heshima,
Chombo bora cha ibada,
Waridi lenye fumbo,
Mnara wa Daudi,
Mnara wa Pembe,
Nyumba ya dhahabu,
Sanduku la Agano,
Mlango wa mbingu,
Nyota ya asubuhi,
Afya ya wagonjwa,
Kimbilio la wakosefu,
Msaada wa wenye uchungu,
Msaada wa Wakristu,
Malkia wa Malaika,
Malkia wa Mababu,
Malkia wa Manabii,
Malkia wa Mitume,
Malkia wa Mashahidi,
Malkia wa Waungama,
Malkia wa Mabikira,
Malkia wa Watakatifu wote,
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili,
Malkia wa uliyepalizwa mbinguni,
Malkia wa Rozari Takatifu,
Malkia wa familia,
Malkia wa amani.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoae dhambi za ulimwengu,
utusamehe, Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoae dhambi za ulimwengu,
utusikilize, Ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoae dhambi za ulimwengu,
utuhurumie.
Utuombee, mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
TUOMBE
Tunakuomba,
Ee Bwana Mungu,
utujalie sisi watumishi wako,
afya ya roho na ya mwili siku zote;
Tuopolewe na mashaka ya sasa,
kwa maombezi ya Maria Mtakatifu, Bikira daima,
ili tupate na furaha ya milele.
Kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
Amina.