Salamu Malkia

Salamu Malkia,
mama mwenye huruma;
uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu.
Tunakusihi ugenini hapa,
sisi wana wa Eva;
tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika,
bondeni huku kwenye machozi.
Haya basi, mwombezi wetu,
utuangalie kwa macho yako yenye huruma;
na mwisho wa ugeni huu,
utuoneshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
Ee mpole,
Ee mwema,
Ee mpendelevu Bikira Maria.