Malaika wa Bwana

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu Maria...
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu Maria...
Neno wa Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu Maria...
Utuombee mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe.
Tunakuomba Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi, tuliojua kwa maelezo ya malaika, kwamba mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko, kwa njia ya Kristu, Bwana wetu.
Amina.
Atukuzwe Baba...