Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli
(Wimbo wa Zakaria)
Lk 1,68-79


Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli! /
Kwani amekuja kuwasaidia
na kuwakomboa watu wake.

Ametupatia Mwokozi shujaa
mzao wa Daudi mtumishi wake,

Aliahidi hapo kale,
kwa njia ya manabii wake watakatifu,

Kwamba atatuokoa kutoka maadui wetu,
na kutoka mikono ya wote wanaotuchukia.

Alisema kwamba atawaonea huruma wazee wetu,
na kukumbuka agano lake takatifu.

Kwa kiapo alichomwapia mzee wetu Abrahamu /
aliahidi kutukomboa kutoka maadui wetu
na kutujalia tumtumikie bila hofu,

Ili tuwe watakatifu na waadilifu mbele yake,
siku zote za maisha yetu.

Nawe mwanangu utaitwa,
nabii wa Mungu Aliye Juu,.

Utamtangulia Bwana
kumtayarishia njia yake;

Kuwatangazia watu kwamba wataokolewa
kwa kuondolewa dhambi zao,

Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma /
atasababisha pambazuko angavu la ukombozi,
litujie kutoka juu,

Na kuwaangazia wote wanaokaa /
katika giza kuu la kifo,
aongoze hatua zetu katika njia ya amani.

Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele. Amina.


Atukuzwe Baba...