Sala ya Kutubu



Namuungamia Mungu Mwenyezi,
na kwa Maria mwenye heri Bikira daima,
na kwa Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu,
na kwa Mtakatifu Yohane Mbatizaji,
na kwa Watakatifu Petro na Paulo Mitumie,
na kwa Watakatifu wote
kwani nimekosa mno
kwa mawazo, kwa maneno, na kwa vitendo,
nimekosa mimi, nimekosa mimi,
nimekosa sana.
Ndiyo maana, namwomba Maria mwenye heri, bikira daima
Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu,
Mtakatifu Yohane Mbatizaji,
Wataktifu Petro na Paulo Mitume,
na Watakatifu wote,
waniombee kwa Bwana Mungu wetu.

Amina.


K. Mungu Mwenyezi awahurumie, awasamehe dhambi zenu,
na awafikishe kwenye uzima wa milele


W. Amina.