Wimbo wa Bikira Maria
(Lk 1,46-55)



Moyo wangu wamtukuza Bwana, /
Roho yangu inafurahi
kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.

Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma /
mtumishi wake mdogo,
hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu,
jina lake ni takatifu.

Huruma yake kwa watu wanaomcha
hudumu kizazi hata kizazi.

Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:
amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

Amewashusha wenye vyeo kutoka viti vyao vya enzi,
akawakweza wanyenyekevu.

Wenye njaa amewashibisha mema,
matajiri amewaacha waende mikono mitupu.

Amempokea Israeli mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake,

Kama alivyowaahidia wazee wetu,
Abrahamu na uzao wake hata milele.


Atukuzwe Baba...