Sala ya Matoleo



Ee Yesu,
kwa mikono ya Bikira Maria,
na kwa maungano na sadaka yako kuu,
ninakutolea sala, matendo,
masumbuko na furaha zangu zote za leo,
kwa ajili ya nia za Moyo wako Mtakatifu,
kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu,
kwa nia za ndugu zangu na rafiki zangu,
na hasa kwa nia za Baba Mtakatifu.

Ee Yesu ufalme wako utufikie.

Amina.