ala ya asubuhi

Ninakuabudu, Mungu wangu,
na ninakupenda kwa moyo wangu wote.
Ninakushukuru, Bwana,
kwa kuniumba, kunikomboa,
kunifanya Mkristu
na kunilinda usiku huu.
Nitakutolea matendo yangu ya leo,
fanyiza kwamba yawe kadiri ya mapenzi yako na kwa ajili ya utukufu wako.
Mama yangu mpendwa Maria nitazame siku hii ya leo.
Malaika mlinzi wangu, unitunze.
Mtakatifu Yosefu na enyi watakatifu wote wa Mungu, mniombee.
Amina.