ala ya Jioni

Ee Mungu wangu, mwishoni mwa siku hii
Nakushukuru kwa moyo wangu wote
kwa neema nyingi nilizopokea toka kwako.
Nahuzunika kwamba sikuzitumia vizuri sana.
Nahuzunika kwa dhambi nilizokutenda.
Unisamehe ee Bwana,
na kwa neema unilinde usiku huu.
Bikira mbarikiwa, Maria, mama yangu mpenzi,
niweke katika ulinzi wako.
Mtakatifu Yosefu, Malaika Mlinzi wangu mpenzi,
nanyi watakatifu wote wa Mungu, mniombee.
Amina.