Malkia wa Mbingu



Malkia wa Mbingu furahi! Aleluya.
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya,

Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, haleluya.

Furahi, shangilia ee Bikira Maria, Aleluya.
Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya.


Tuombe.

Ee Mungu Baba yetu,
ulipenda kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana yetu Yesu Kristu, mwanao;
fanyiza, twakuomba, kupitia Bikira Maria mamaye,
tupate nasi furaha za uzima wa milele.
Kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

Amina.