Uje Roho Mtakatifu



Uje Roho Mtakatifu
Uzienee nyoyo za waumini wako
uwajaze moto wa mapendo yako.

V. Mtume Roho wako vitaumbwa upya
R. Na nchi itageuka.


Tuombe

Ee Mungu, uliyefundisha nyoyo za waumini wako, kwa kuwaletea mwanga wa Roho Mtakatifu, tunaomba utuongoze kwa yule roho, tupende yaliyo mema na tupate daima faraja zake. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

Amina.