The following audio files will be sent:
(* Optional)
sw_segno_croce.mp3
+ Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
sw_eterno_padre.mp3
Baba wa milele, ninakutolea mwili na damu, Roho na Umungu wa Mwanao mpenzi sana, Bwana wetu, Yesu Kristu, kwa kulipia dhambi zetu na dhambi za ulimwengu mzima.
sw_per_la_sua.mp3
Kwa ajili ya mateso yake makali, utuhurumie sisi na ulimwengu mzima.
sw_santo_dio.mp3
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu Mwenye Enzi, Mtakatifu Usiyeweza Kufa, utuhurumie sisi na ulimwengu mzima.
sw_sangue_e_acqua.mp3
Ee Damu na Maji, vilivyobubujika kutoka kwenye Moyo wa Yesu kama chemchemi ya Huruma kwetu, Nakutumainia!
sw_credo.mp3
KANUNI YA IMANI
sw_pater.mp3
Baba yetu
sw_ave.mp3
Salamu Maria
sw_gloria.mp3
Atukuzwe Baba
sw_salve_regina.mp3
Salamu Malkia
sw_Litanie.mp3
Litania ya Loreto
sw_gesu_mio.mp3
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji zaidi Huruma Yako.
sw_o_dio.mp3
Ee Mungu uje kunisaidia. Ee Bwana unisaidie hima.
sw_regina_pace.mp3
Maria, Malkia wa Amani utuombee.
sw_intenzioni_papa.mp3
Sala kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu...
sw_gioia1.mp3
Fumbo la Kwanza la Furaha
Malaika anampasha habari Maria kwamba atakuwa Mama wa Mungu
Tunda la fumbo: Unyenyekevu
sw_gioia2.mp3
Fumbo la Pili la Furaha
Maria anamtembelea Elizabeti
Tunda la fumbo: Upendo kwa jirani
sw_gioia3.mp3
Fumbo la Tatu la Furaha
Yesu anazaliwa Bethlehemu
Tunda la Fumbo: Ufukara
sw_gioia4.mp3
Fumbo la Nne la Furaha
Yesu anatolewa hekaluni
Tunda la fumbo: Utii kwa sheria ya Mungu
sw_gioia5.mp3
Fumbo la Tano la Furaha
Yesu anakutwa Hekaluni
Tunda la Fumbo: Furaha ya kumpata Yesu katika maisha yako
sw_luce1.mp3
Fumbo la Kwanza la Mwanga
yesu anabatizwa mtoni Yordani
Tunda la Fumbo: Utayari kwa Roho Mtakatifu
sw_luce2.mp3
Fumbo la Pili la Mwanga
Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana
Tunda la Fumbo: Kwa Yesu Kupitia Maria
sw_luce3.mp3
Fumbo la Tatu la Mwanga
Yesu anatangaza ufalme wa Mungu
Tunda la Fumbo: Toba na Kumtumaini Mungu
sw_luce4.mp3
Fumbo la Nne la Mwanga
Yesu Anageuka Sur
Tunda la Fumbo: Tamaa ya Utakatifu
sw_luce5.mp3
Fumbo la Tano la Mwanga
Kuwekwa kwa Ekaristi Takatifu
Tunda la Fumbo: Kuabudu
sw_dolore1.mp3
Fumbo la Kwanza la Uchungu
Yesu anatoka jasho la damu
Tunda la Fumbo: Sikitiko timilifu
sw_dolore2.mp3
Fumbo la Pili la Uchungu
Yesu anapigwa mijeledi
Tunda la Fumbo: Usafi wa moyo
sw_dolore3.mp3
Fumbo la Tatu la Uchungu
Yesu anavikwa taji la miiba
Tunda la Fumbo: Ujasiri katika maadili
sw_dolore4.mp3
Fumbo la Nne la Uchungu
Yesu anabeba msalaba wake
Tunda la Fumbo: Subira
sw_dolore5.mp3
Fumbo la Tano la Uchungu
Yesu anasulibiwa na kufa msalabani
Tunda la Fumbo: Ustahimilivu
sw_gloria1.mp3
Fumbo la Kwanza la Utukufu
Yesu anafufuka
Tunda la Fumbo: Imani
sw_gloria2.mp3
Fumbo la Pili la Utukufu
Yesu anapaa mbinguni
Tunda la Fumbo: Matumaini
sw_gloria3.mp3
Fumbo la Tatu la Utukufu
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume
Tunda la Fumbo: Mapendo
sw_gloria4.mp3
Fumbo la Nne la Utukufu
Bikira Maria anapalizwa mbinguni
Tunda la Fumbo: Neema ya kifo chema
sw_gloria5.mp3
Fumbo la Tano la Utukufu
Bikira Maria anatawazwa Malkia Mbinguni
Tunda la Fumbo: Tumaini katika maombezi ya Maria
OPCIONAL:
sw_gioia1v.mp3 (*)
«Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi.» (Lk 1:26-27).
sw_gioia2v.mp3 (*) (*)
«Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yudea. Huko, aliingiaa katika nyumba ya Zakaria, akamsalimu Elizabeti. Mara tu Elizabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elizabeti akaruka. Naye Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akasema kwa sauti kubwa, "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa."» (Lk 1:39-42).
sw_gioia3v.mp3 (*)
«Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe. Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria. Basi, wote waliohusika walikwenda kuhesabiwa kila mtu katika mji wake. Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi. Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito. Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia, akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.» (Lk 2:1-7).
sw_gioia4v.mp3 (*)
«Siku nane baadye, wakatiwa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana. Katika sheria ya Bwana imeandikwa: 'kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana." Pia walikwenda ili watoe sadaka: Hua wawili au makinda mawili ya njiwa kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana.» (Lk 2:21-24).
sw_gioia5v.mp3 (*)
«Wazazi wake walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa destri. Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima.» (Lk 2:41-47).
sw_luce1v.mp3 (*)
«Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipanda kutoka majini, na tazama, mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye"» (Mt 3:16-17).
sw_luce2v.mp3 (*)
«Siku ya tatu kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya, na mama yake Yesu alikuwepo; Yesu pia alikuwa amealikwa kwenye arusi hiyo pamoja na wanafunzi wake. Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, "Hawana divai." Yesu akamjibu, "Mama, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia bado." Mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambia, fanyeni."» (Jn 2:1-5).
sw_luce3v.mp3 (*)
«"Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili"» (Mk 1:15).
sw_luce4v.mp3 (*)
«Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.» (Mt 17:1-2).
sw_luce5v.mp3 (*)
«Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, "Twaeni, mle; huu ni mwili wangu"» (Mt 26:26).
sw_dolore1v.mp3 (*)
«Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali." Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko. Hapo akawaambia, "Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami." Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe."» (Mt 26:36-39).
sw_dolore2v.mp3 (*)
«Basi Pilato akamtwaa Yesu, akamchapa mijeledi. Askari wakasuka taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, wakamvika vazi la rangi ya zambarau; wakamjia na kusema, "Salamu, Mfalme wa Wayahudi!" wakampiga makofi.» (Jn 19:1-3).
sw_dolore3v.mp3 (*)
«Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima. Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu. Kisha wakasokota taji la miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!"» (Mt 27:27-29).
sw_dolore4v.mp3 (*)
«Wakamlazimisha mtu mmoja aliyekuwa anapita, Simoni wa Kirene, baba yake Aleksanda na Rufo, abebe msalaba wake. Wakafika mahali paitwapo Golgotha, maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa.» (Mk 15:21-22).
sw_dolore5v.mp3 (*)
«Walipofika mahali paitwapo, "Fuvu la Kichwa," ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto. Yesu akasema, "Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya."...Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likaifunika nchi yote mpaka saa tisa, na pazia lililokuwa limetundikwa hekaluni likapasuka vipande viwili. Yesua akalia kwa sauti kubwa: "Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu." Alipokwisha sema hayo, akakata roho.» (Lk 23:33-46).
sw_gloria1v.mp3 (*)
«Siku ya kwanza ya juma, alfajiri mapema, walikwenda kaburini wakiwa wamebeba manukato waliyoandaa. Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, lakini walipoingia hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu. Walipokuwa wakishangaa, watu wawili waliovaa mavazi ya kung'aa walitokea karibu nao; nao waliogopa, wakainamisha nyuso zao. Wale watu wakawaambia, "Mbona mnatafuta aliye hai kati ya wafu? Hayupo hapa, amefufuka."» (Lk 24:1-5).
sw_gloria2v.mp3 (*)
«Basi, Bwana Yesu, baada ya kusema nao, alipaa kwenda mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.» (Mk 16:19).
sw_gloria3v.mp3 (*)
«Siku ya Pentekoste ilipowadia, walikuwa wote pamoja mahali pamoja. Ghafula pakatokea sauti kutoka mbinguni kama mvumo wa upepo wa nguvu, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wamekaa. Kukawatokea ndimi kama za moto, zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha mbalimbali kama Roho alivyowajalia kunena.» (Mdo 2:1-4).
sw_gloria4v.mp3 (*)
«"Tangu sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa, kwa sababu yeye aliye na uwezo amenitendea mambo makuu"» (Lk 1:48-49).
sw_gloria5v.mp3 (*)
«Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!» (Ufu 12:1).
Submit audio files
here
THANKS!!!
Created with Mobirise
Free Web Page Designing Software